Fahamu Warembo Waliofanikiwa Zaidi Katika Nyanja Mbalimbali Tanzania

1.Jokate mwegelo

download latest music    

Safari yake ya mafanikio ilianza kwa kushiriki mashindano ya u-miss .Ni mrembo  mjasiriamali anayeingia katika kundi la watu waliofanikwa hasa kupitia kampuni yake ya Kidoti,amekuwa akirudisha fadhila katika jamii kupitia sekta mbalimbali, kwanza alianza na kutoa misaada kwa wasusu mitaani, lakini pia alikuja na kampeni ya kusaidia utoaji wa vifaa vya shule kwa wasichana wanaoishi katika mazingira magumu.Jokate pia alishawahi kutoa msaada wa kujenga kiwanja cha mpira katika shule ya Jangwani.

2.Faraja Nyalandu

Amekuwa ni mfano wa kuigwa wa wasichana wengi katika jamii, Faraja ametoa mchango mkubwa sana katika sekta ya elimu kupitia project yake ya Shule Direct

3.Doris mollel

Amekuwa akitoa msaada mkubwa sana katika sekta ya afya hasa kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya umri wao(NJITI), chini ya Dorris Mollel Foundation, ameweza kutoa mashine pamoja na vitanda kwa wahitaji hao.Alianza kama Miss Singida mwaka 2014, na baadae Miss Tanzania namba tatu.

4.Flaviana matata

Mwanamitindo anayeishi nje ya nchi, safari yake ya mafanikio ilianza pale aliposhiriki Miss Universr mwaka 2007,amekuwa akisaidia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu chini ya Flaviana Matata Foundation.

5.Jenniffer Bash

Mrembo aliyeamua kuangalia fursa katika sekta ya kilimo, wengi wanamjua kaka mama Alaska, ikiwa Alaska ni jina la kampuni yake.aliona ni bora kushirikianana wakulima wa mashambani ili kuweza kuagawana faida na kunufaisha jamii pia.Kwa sasa kampuni yake inauza mayai, mchele na mafuta.

6.Nasreen Kareem

Alikuwa mshindi wa Miss Tanzania mwaka 2008,kwa sasa amejikita zaidi katika maswala ya urembo hasa wa asili akishirikia na wanawake wa jamii za kimasai katika utengenezaji wa bidhaa za shanga.Duka lake limekuwa ni moja ya maduka makubwa yanyotangaza bidhaa za asili.

7.Jackline Ntuyabaliwe

Ni mrembo aliyepitia vipaji vingi mpaka kufika hapa, alianza na kushirki U-misss mwaka 2000, na kuwakirisha Tanzania Miss World. Alishapita kwenye kuimba ,kwa sasa amejikita katika ubunifu.Ameshashinda tuzo ya designer bora wa vitu vya thamani.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.