Loading...

Faiza Ally Athibitisha Kumaliza Bifu Lake na Sugu

June 13, 2018 at 09:58
Faiza Ally Athibitisha Kumaliza Bifu Lake na Sugu

Muigizaji wa Bongo movie Faiza Ally na mzazi mwenzake ambaye ni  Mbunge wa Mbeya Mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ wameonekana kumaliza bifu lao.

Faiza na Sugu wameshawahi kurushiana maneno Kwenye mitandao ya kijamii mara kwa mara na hata kufikia hatua ya Faiza kumtukana matusi ya nguoni mzazi mwenzake.

Loading...

Hali ilikuwa mbaya baina yao hadi kufikia hatua ya Sugu kutopewa nafasi ya kumuona binti yao anayeitwa Sasha.

Lakini hivi sasa inaelekea hali ni shwari kwani Faiza ameweka picha Mtandaoni zinazomuonyesha Sugu akiwa na binti yake ambaye ameenda kumtembelea mkoani Mbeya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza aliweka picha ya Baba na mtoto na kusindika na ujumbe mfupi ili kudhihirisha kuwa hivi sasa hana tatizo na mzazi mwenzake huyo.

Faiza ameandika:

Najisikia vizuri kuwaona Baba na mtoto pamoja tena…. Nawapenda sana”

.

 

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…