Faiza Ally Awapa Somo Mabinti Kuhusu Wanaume

Msanii wa Filamu za Bongo Movie na mzazi mwenza wa mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi, Faiza Ally amefunguka na kuwapa somo watoto wa kike kuhusu wanaume.

Faiza amewasihi mabinti kutowaendekeza wanaume kiasi cha kukubali mapenzi yawarudishe nyuma kimaendeleo.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza amewapa ushauri wasichana na kujitoa mfano na kuweka wazi kuwa amerudishwa nyuma kimaendeleo na mapenzi na sasa anakuwa kama anaanza upya:

Kama kuna binti anasoma haya naomba nikwambie tu tafuta maisha usikubali kuyumbishwa akili Wanaume wanaume wanarudisha wanawake nyuma mara nyingi sana.

Mimi ni mmoja ya Wanawake waliorudishwa nyuma na mapenzi na kwa sasa ni kama naanza upya kuna wakati mwingine nawish ningeona ya mbele ili nijiokoe lakini siri ya maisha anaijua Mungu pekee lakini pamoja na hayo yote kama bado unaishi unayo nafasi nyingine usikate tamaa”.

Faiza hakumtaja mwanaume aliyemrudisha nyuma kimaendeleo lakini siku za nyuma ameshawahi kumlaumu Baba mtoto wake Sugu kwa kumpumbaza kimapenzi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.