Gigy Money Afungukia Uwamuzi Wake Wa Kumuachia Mtoto Wema Sepetu

Video vixen na msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefungukia uamuzi Wake wa kumuacha Mtoto Wake na Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu.

Wiki iliyopita Kupitia ukurasa wake wa Instagram Gigy Money aliweka wazi kuwa kabla ya kusafiri kwenda kufanya shoo mkoani Mwanza ameamua kumuacha binti yake na Wema kwani anaamini ni mama mzuri na anapenda sana watoto.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Gigy Money aliyekuwa safarini jijini Mwanza huku akimwacha mwanaye kwa Wema jijini Dar, Gigy alisema amemuona Wema ana upendo na pia anapenda watoto hivyo akaamua kumuachia na kwenda kutafuta maisha akijua yupo mikono salama.

Namuomba Mungu amjalie Wema apate mtoto maana ni mama mwenye upendo ndiyo maana nimemuachia Maira amlee na ninajua atakuwa kwenye mikono salama“.

Wema ameshaweka wazi mapenzi yake kwa watoto licha ya kushindwa kupata Mtoto Wake wa kumtaka mwenyewe.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.