Gigy Money Amjia Juu Hemed Phd

Video queen maarufu ambae hivi  sasa ameingia pia katika muziki na anafanya vizuri pia katika tasnia hiyo, amemjia juu msanii mwenzie wa bongo fleva na kumwambia kuwa msanii huyo amezeeka,hemed ambae pia alishahawahi kumuoongelea  vibaya msanii huyo wa kike ameambiwa kuwa kwa sasa hayupo vizuri kichwani  kwa babu ya kuzeeka kwake na hata hivyo hana ela ya kumuongelea msanii kama yeye.

Akiongea na moja ya waaandishi wa habari wa East Africa , Gigy Money amesema kuwa kwa sasa hivi yeye hawezi kuzungumza chochote kuhusu Hemed Phd kwa sababu Hemed kichwani hayupo vizuri sana na hata kifedha amefulia hivyo hata yeye hawezi kukubali kuongelewa chochote na Hemed Phd.

download latest music    

yeye amesema hana hadhi ya kuniongelea mtu kama mimi wakati mimi ndo simjui kabisa  kwanza nimemsahau,nahisi sahivi atakuwa mzee sana, na kama unavyojua kuwa watu wazee wanapotezaga sana  kumbukumbu,na kwakweli hana tu hadhi ya kuniongelea mtu kama mimi aisee,kwanza hana ela, maskini tu yule” aliongea Gigy Money

Baadhi ya wasanii wamekuwa wakiingia katika migogoro na wasanii wenzio mara nyingi bila kuwa na sababu yoyote ya msingi huku baadhi ya maneneo wanayorushiana yanakuwa  yanalenga maisha binafsi bila kujenga kazi zao za muziki.Bifu kati ya Hemed na Gigy Money halitakuwa la kwanza kwa wasanii kwa sababu wasanii wengine wamekuwa na mgogoro ambao mwisho wa siku inapunguza mashabiki lakini pia inahathiri kazi zao za muziki.

Kwa msanii Gigy Money ambae kwa sasa ndio ameanza kuchipikua na kufanya vizuri katika muziki, anapswa kuwa moja ya watu wenye marafiki na kuwa na watu karibu ilikutengeneza mashabiki wengi zaidi, lakini yeye ni mmoja ya wasanii wenye bifu na watu wngi zaidi na kuwa mmoja wa watu wanaotupiana na maneno na mashaabiki zao sana katika mitandao.

kwa sasa  Gigy Money anafanya vizuri katika moja ya vibao vyake vipya kiinachojulikana kwa jina la Papa, na kimepokelewa vizuri na mashabiki pia.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.