Gigy Money Aweka Wazi Kuwa Yeye Ni Wa Gharama (Video)

Video vixen maarufu Bongo na asiyeisha vituko Gigy Money aliyegeukia fani ya muziki ameweka wazi na kudai kuwa yeye ni msanii wa gharama.

Gigy money anayefanya vizuri kwenye stesheni mbali mbali za redio na wimbo wake wa ‘Nampa papa’ amefunguka na kudai dau lake la kuperfom ni kubwa tofauti na wasanii wengine wengi.

download latest music    

Gigy Money aliweka wazi kuwa kama kuna promota anataka kumkodi kwaajili ya kuperfom klabu au popote dau lake la chini linaanzia milioni mbili na kuendelea.

Kuanzia sahivi na-perfom stejini kwa dau la kuanzia milioni mbili, Nampa papa its a hit song, bila milioni mbili siwezi kutoa papa stejini its a hit song”.

Ni siku tu za hivi karibuni kwenye mahojiano na Lil Ommy, Gigy Money aliamua kuwaacha watu midomo wazi baada ya kudai kuwa weaving/ nywele yake aliyoshonea kichwani imemgharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni sita.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.