Gigy Money na Nandy Wanapaswa Kuwa Jela :-Musiba

Mwanaharakati wa gazeti moja nchi, amefunguka na kusema kuwa kwa wasanii kama Nandy na Gigy Money  wanatakiwa kupewa adhabu kali kwa kuwa wamekuwa watovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili kwa njia ya mitandao.

Musiba anasema kuwa kama serikali ilishindwa kumfunga Nandy na Gigy money basi walitakiwa kuwapa fine ya milioni mia moja kwanza  ili kuwafunza maadili juu ya ufanyaji wao kazi katika sanaa.

download latest music    

Haya yanakuja kutokana na kuwa na wimbi la wasanii wengi wanaoamua kuvunja sheria ya mitandao kwa kuweka video chafu katika mitandao ya kijamii ikiwa ni kosa la jinai.

Musiba anasema “Yan kama Gigy money anatakiwa kufungwa tu jela, lakini wakienda BASATA utawasikia tu tumewasamehe tena kwa kubana pua, tuna watoto wanamaliza darasa la saba na wanaingiakatika mitandao wataona nini huko, na hata huyo nandy basi kama hawawezi kumfunga hata wampige fine ya milioni 100.’

Na hapa karibuni wasanii wa kike wamekuwa wakifanya kosa hilo na watu wengi wametaka wasanii hao kupewa adhabu za kuwafaa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.