“Hamisa Anapata Mafanikio Baada Ya Kuachana na Diamond”-Mama Mobetto

Mama mzazi wa mwanamitindo na msanii Hamisa Mobetto anayejulikana kama Shufaa Rutiginga maarufu kama Mama Mobetto amefunguka na kuweka wazi kuwa kilichokuwa kinamkwamisha mwanaye ni mapenzi lakini baada ya kuachana nayo mambo yanamnyookea.

Hamisa Mobetto aliachana na mzazi mwenzake Diamond Platnumz ,miezi michache iliyopita na tangia hapo amekuwa akipata madili makubwa kama ubalozi wa makampuni na hata kutoa wimbo wake wa kwanza unaozidi kufanya vizuri kwenye Youtube.

download latest music    

Siku chache baada ya Hamisa kuonekana akifanya shoo nchini Marekani mama Mobetto ameibuka na kuweka wazi kuwa mwanaye amefanikiwa baada ya kuyaeweka kando mambo ya mapenzi yaliyokuwa yanampotezea muda na kuamua kupiga kazi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi Mchanganyiko, Mama Mobetto amesema siri kubwa ya mwanaye kuonekana mambo kumwendea vizuri baada tu ya kuachana na Diamond ni kwa sababu amekuwa msikivu kwa kila jambo analomwelekeza.
Aliendelea kusema kwamba amekuwa akimshauri na kumwelekeza Mobeto mambo mengi sana yanayohusiana na maisha na anamshukuru Mungu kwani kwa sasa amekuwa ni mtoto msikivu sana na ameona faida yake kwani amekuwa akipata kazi mbalimbali nje ya nchi.

Namshukuru Mungu sana kwa kila jambo kwani mwanangu baada ya kuachana na ishu za mapenzi amekuwa msikivu, anasikiliza na kuzingatia kile ninachomwambia kama mama yake na ndiyo maana anafanikiwa na anazidi kutusua kila siku”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.