Hamisa Kuingia Kwenye Fani Ya Uigizaji

Anajulikana zaidi katika uuzaji wa nyango katika video za wasanii mbalimbali ikiwemo ile ya Salome kutoka kwa msanii Diamond Platinumz, kumbe anaweza kufanya kazi nyingi tofauti na hizo.Video queen  mwenye maarufu  wake ambae kwa sasa anazidi kuwa maarufu zaidi kutokana na scandal nyingi ziinazomkabili  hasa katika mambo yake ya kifamilia na mahusiano ,Hamisa Mobeto  amethibitisha kuwa na kipaji kingine cha kuigiza baada ya kushirikishwa katika filamu mojawapo inayotegemwa kutoka hivi karibuni.

Katika ukurasa wake wa instagram, Hamisa mobeto aliposti picha ya movie iyo inayoitwa Zero Player na kusema kuwa yeye pia atakuwa mmoja wa mastaa wataoshiriki filamu iyo inayotegemewa kuchezwa na wasanii wengine wakubwa kutoka Afrika ya Kusini, Ghana,Nigeria na Cameroon huku ikiwa na mazingira ya kuigizia kutoka Tanzania na Afrika ya Kusini.

download latest music    

Uzinduzi wa filamu mpya iliyofanyika South Africa na tanzania ,ikinishirikisha mimi na mastaa wengine kutoka Afrika ya Kusini ,Ghana, Nigeria, & Cameron….Inaatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.Tukae tayari kwa mkao wa kula” aliandika Hamisa Mobeto na kuwaomba mashabiki wake wake mkao wa kula wakisubiri kumuona nini anaenda kufanya humo ndani. Hii pia itakuwa ni moja ya nafasi nzuri kwa Hamisa kuonyesha kipaji chake icho.

Hamisa ni mama wa watoto wawili mmoja wa kike aliyezaa na boss ya stesheni moja ya Radio na Tv, na wa pili akiwa amezaaa na Diamond Platinumz , ambae bado wana migogoro mpaka hivi sana kuhusu mtoto huyo.

Hamisa kwa sasa amekuwa katika scandal ya kugombana na mwanamke wa mwanaume aliyezaa nae(Zari) ambae pia ni msanii mkubwa Tanzania Diamond Platinumz, lakini pia hivi karibuni amekuwa na majibizano ya kimtandao na mwanadada mrembo kutoka Kenya anaejulikana kama Queen V.

Pamoja na kukumbwa na mambo mengi katika mtandao, Hamisa Mobeto bado anaonekana kuwa imara kabisa na kuendelea na kazi zake, ambapo wiliendi hii alikuwa na sherehe ya mwanae mdogo wakiume na baada ya hao aliwasili nchini kenya kwa ajili ya ‘special appearance’ katika event aliyoalikwa ikiwa ni kama moja ya kazi anazofanya kwa sasa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.