Hamisa Mobetto ampa mtoto wake jina Kiowa, Abdul Naseeb

Hamisa Mobetto ambaye ni video vixen na model amewaacha wengi wakijiuliza maswali baada ya kumpa mtoto wake jina la Abdul Naseeb. Jina hili limezua maswali mengi huku wengi wakidai kuwa hii ni dhibitisho tosha kuwa ni mtoto wa Diamond Platnumz.

Abdul Naseeb ambaye alizaliwa Agosti 8 mwaka huu amekuwa akifichwa na Hamisa Mobetto ambaye bado anangoja kuonyesha sura ya baby Dully Dee.

download latest music    

Kwa sasa Hamisa Mobetto amebadilisha jina la akaunti ya Instagram kutoka ‘Tanzania Baby’ na kuandika ‘Abdul Naseeb’. Hata hivyo bado tunangoja kusikia atakocho sema Diamond Platnumz kwa sababu mama yake (mama Diamond) wiki iliyopita aliambia Shalawadu Clouds TV walionekana katika hospitali ambayo alijifungilia mrembo huyo.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua