Hamisa Mobetto Awataka Mashabiki Zake Wake Wavumilivu

Mwanamitindo na msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto amefunguka na kuwataka mashabiki zake kumvumilia katika kipindi hiko ambacho yupo katika Mahaba mazito.

Hamisa Amezidi kukamata headlines kwenye mitandao ya kijamii tangu aliposafiri kwenda nchini Marekani kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki na kupata Mpenzi mpya anayejulikana Kama Josh Adeyeye.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Hamisa alisema kuwa anajua watu wengi wangependa kumuoana anarudi nyumbani sasa hivi wajue ni kitu gani kinaendelea lakini amewaomba watulie kila kitu ambacho wananakitarajia kutoka kwake watakiona.

Najua watu wengi mnataka kujua nikija nyumbani inakuwaje au mambo yangu yatakuaje mimi nimewaomba mtulie tuli mambo yataenda kama mnavyoniombea na yameshakuwa kabisa”.

Hamisa amezidi kufanya Vizuri Baada ya kuachia wimbo wake siku ya jana unaoitwa ‘Tunaendana’ ambao umeshika namba moja kwenye mtandao wa YouTube.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.