Harmonize Adai Kuwa Yeye na Diamond Wanamiliki Hisa Sawa Sawa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Harmonize amefunguka na kuweka wazi yeye na Bosi wake  Diamond Platnumz wanamiliki hisa pasu kwa pasu kwenye kampuni ya Zoom Production.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha redio cha A FM cha jijini Dodoma, Harmonize ameanika ukweli ambapo amesema kuwa wote wawili wamegawana hisa sawa kwa sawa.

download latest music    

Wazo la kuanzisha Production company ni langu na nilipolipata nilienda Africa ya kusini na Marekani kununua kamera na baadae nikaja kusambaa Diamond, Bro! mimi naona tunapoteza hela nyingi sana kwenye video, mimi nimepata wazo la kuanzisha kampuni ya Video Productions wewe unaonaje?“

Harmonize amesema Diamond akakubali wazo hilo na kwa kuwa alikuwa ameshanunua kila kitu alivyorudi Bongo alimrudishia nusu ya manunuzi na kwa muda huo anasema kuwa alikuwa ameshmtafuta Director Kenny.

Zoom Production ni moja ya kampuni zinazofanya vyema kwenye ulimwengu wa Burudani na haimilikiwi na Diamond pekee ilivyoaminika hapo awali bali na Harmonize pia ana mkono mule.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.