Harmonize Akana Mahusiano Yake na Sarah Mzungu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutokea kwenye Label kubwa Bongo WCB, Harmonize amejikuta akijikanyaga Baada ya kuulizwa kuhusu Mpenzi Wake na kuishia kukana mahusiano yake na Sarah Mzungu.

Harmonize yupo nchini Nigeria na siku ya jana,  Jumatatu Februari 25, 2019 alitembelea kwenye kituo cha radio cha The Beat 99.9 FM cha jijini Lagos kwa ajili ya Media Tour.

download latest music    

Kwenye mahojiano hayo, Harmonize aliulizwa maswali kadhaa na swali la kwanza lilikuwa ni “Tunamuona mwenzio Diamond yupo na Tanasha vipi wewe upo single?”.

DAHH MIMI? NIPO SINGLE NA NATAFUTA PIA…HAPANA NATANIA SIPENDI KUZUNGUMZIA SANA MAHUSIANO YANGU, UNAJUA MIMI MASHABIKI WANGU NI WANAWAKE NINAVYOJIBU WENGINE WATAJISIKIA VIBAYA”.

Kiukweli ni kwamba Harmonize yupo kwenye mahusiano ya muda mrefu na Mpenzi wake Sarah ambaye pia yupo kwenye moja ya nyimbo zake ambayo ipo kwenye EP yake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.