Harmonize Amshauri RayVanny Amsamehe Mpenzi Wake Fahyma

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka WCB, Harmonize ameingilia kati na igomvi unaoendelea mtandaoni kati ya msanii mwenzake kutoka WCB Rayvanny na mzazi mwenzie Fahyma.

Siku ya Jumatatu Rayvanny na Fahyma walianzisha balaa mtandaoni na kutrend baada ya kulete matatizo yao mtandaoni na Rayvanny kumtosa mama mtoto wake huyo na kumwambia aache kutumia jina lake.

download latest music    

Kisa cha Rayvanny kumtosa Fahyma hakijajulikana lakini kumekuwa na tetesi kuwa mini mkata kamba aliyeingilia penzi lao ni michepuko ingawa haijajulikana sana ni nani kati yao mwenye michepuko kwani kila mmoja ameonekana kumtupia lawama.

Mpaka hivi sasa hakuna taarifa kabisa ya uhakika kuhusu nini kinaendelea lakini tangu Jumanne Rayvanny amekuwa akilalamikia kitendo cha kumkosa mwanae Jaden, yaani inavyoelekea Rayvanny na Fahyma hawako wote na Fahyma ndo yuko na mtoto wao.

Sasa Jana rafiki wa Rayvanny na msanii mwenzie Harmonize aliibuka na kumpa ushauri na kumuomba wayamalize matatizo yao yanayowakabili na waweze kumlea mtoto wao:

Lakini hapana kaka tusifike huko mtoto anahitaji matunzo ya baba na mama tumlaani shetani kwani mwenzio kateleza”.

Baada ya Harmonize kuandika maneno hayo kwenye ukurasa wa Rayvanny wa Instagram watu wengi walitafsiri maneno hayo kama Fahyma ndiye mwenye makosa kwani Harmonize alikuwa anamuombea msamaha, lakini badala yake Rayvanny alipuuza maneno yake na kumwambia Harmonize aache unafki

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.