Harmonize Aomba Radhi Baada Ya Shoo Yake Kubuma Nchini Kenya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutokea katika label ya WCB, Harmonize amejikuta katika wakati mgumu baada ya shoo yake iliyokuwa ifanyike siku ya jana El Derot nchini Kenya kutofanyika na hivyo kulazimika kuomba radhi mashabiki zake.

Sakata hilo lilitokea baada ya Harmonize kushindwa kupanda jukwaani kutumbuiza baada ya Promota aliyemleta kushindwa kumalizia mkwanja wake kama walivyopatana.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameandika ujumbe wa kuwaomba radhi mashabiki ambao walitoa pesa nyingi kununua tiketi lakini wamejikuta wakikosa shoo kutoka kwa Harmonize;

BINAFSI NAJUA KIASI GANI PESA INATAFUTWA KWA UGUMU BUT KWA MAPENZI YENU MLIJITOA KUJA KUNI SUPPORT SIO KWASABABU MIE NI SPECIAL SANA….!!! NI KWA UPENDO WENU TUU ILA KILICHONISIKITISHA NI PROMOTERS KUCHUKUA PESA ZA WATU WASIO PUNGUA 4000K THEN WAKASHINDWA KUJA KUMALIZIA PAYMENT ILIYOBAKI NA KUKIMBIA HII INAUMIZA SANA…!! (1) NI DALILI YA KUNIVUNJIA HESHIMA NA UAMINIFU KWA MASHABIKI ZANGU (2) IMENIUMIZA KUONA WATU WALIOJITOA KULIPA VIINGILIO VYAO JUST FOR ME WANADHULUMIWA MWISHO KABISA…!!! NISEME SAMAHANI #ELDORET ?? NEXT TIME NITAHAKIKISHA TUMELIPWA DOO YOTE KABLA NI COME TRUST ME I’M SO….!!! DISAPPOINTED AND I LOVE YOU ❤ AND I WAS EXTRA READY ?? I DID#SOUNDCHECK AND EVERYTHING THIS IS TO BAD”.

Harmonize siyo msanii wa kwanza kuwanyooshea vidole mapromota feki kutoka nchini Kenya kwani miezi michache iliyopita tu msanii kutoka Nigeria Tiwa Savage alilalamika na prom0ta feki pia.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.