Harmonize: Namchukulia Wolper Kama Shabiki Wangu Tu

Msanii wa Bongo fleva maarufu kama Harmonize ameibuka na kudai kuwa anamchukulia Wolper kama shabiki wake tu na hakuna kingine.

Mwanzoni mwa wiki hii Jacqueline Wolper, ambaye ni mpenzi wa zamani wa Harmonize na Sarah, ambaye ni mpenzi wa sasa wa Harmonize waliingia katika vita kali ya maneno mtandaoni baada ya Sarah kudai kuwa Wolper bado anamtaka Harmonize. Sarah alivujisha meseji za Wolper mtandaoni na kupelekea Wolper kuchefukwa hivyo kumwambia Sarah kuwa alimuazima Harmonize kwa muda tu anaweza kumchukua muda wowote.

download latest music    

Baada ya hapo Wolper alianza kujirekodi anaimba wimbo mpya wa Harmonize unaotamba hivi sasa ‘Shulala’ na hivyo kupelekea minong’ono ya watu kuwa Harmonize na Sarah wameachana na Wolper kamchukua tena Harmonize kwani alimwambia siku nikimtaka Harmonize namchukua tena.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na XXL ya Clouds Fm, Harmonize aliweka wazi kuwa anashukuru mchango mkubwa wa Wolper katika nyimbo yake mpya kwani amejirekodi video mbili akionekana akifurahia wimbo huo.

Nadhani mwanzo ilikuwa ni hasira tu, nashukuru kuona mchango wa Wolper kwani namchukulia kama shabiki wangu tu”.

Pia kwenye mahojiano hayo Harmonize aliweka wazi mipango yake ya kuupeleka mziki wake kimataifa zaidi kwani hivi karibuni anategemea kusafiri kwenda Ghana kwaajili ya kurekodi video ya wimbo aliomshirikisha msanii Sarkodie kutoka Ghana, huu ni muendelezo tu wa mafanikio ya Harmonize kwani wimbo wake huu mpya wa ‘shulala’ amemshirikisha msanii Mkubwa kutoka Nigeria, Korede Bello.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.