Loading...

Harmorapa aendelea na vituko vyake… Sahi ni Kiingereza tu!

April 20, 2017 at 15:13
Harmorapa aendelea na vituko vyake… Sahi ni Kiingereza tu!

Harmorapa ni mchekeshaji kwani mara nyingi ametawala vichwa vya habari kwasababu ya vituko vyake wala si muziki wake.

Rapper huyo anajulikana sana kwa vioja anazopenda kutoa kila mara anapohojiwa kwenye redio ama kwa runinga ama ata atokeapo kwa umma.

Akiongea na mashabiki katika mtandao wa Facebook wa EATV, Harmorapa alikiri kuwa Kiingereza kinampiga chenga.

Hii ni baada ya msanii huyo kuwafanya mashabiki kupasuka kwa kicheko kikubwa  baada ya kujibu swali pasivyo alipoulizwa kwa Kiingereza.

“Wewe ni mwanaume wa aina gani?” Harmorapa aliulizwa kwa Kiingereza.

“Mimi ni strong woman,” Harmorapa alijibu.

Alipoulizwa kama anaelewa Kiingereza vizuri alikiri kuwa anaufahamu lakini kuongea ndo tatizo kwake.

“Lugha ya Kiingereza naifahamu vizuri lakini ile kuongea ongea ndiyo siwezi”

 

Leave a Reply

Be the First to Comment!

avatar
wpDiscuz

in Music
Loading...
Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere