Harmorapa akana kumdiss Majani kwenye wimbo wake mpya

Image: Harmorapa

Rappa kutoka bongo, Harmorapa ameachia nyimbo mpya itwaayo Ajitokeze hivi karibuni lakini wimbo huo umezua ngumzo mitandaoni kwani Harmorapa anasemekana kuwa alimdiss aliyekuwa meneja wake wa zamani, P Funk Majani. Kwenye wimbo huo anaskikaa kisema;

download latest music    

“Nishakuwa mfagizi chini ya miti, nazijua kero za majani, maana majani hayafadhiliki, ndiyo maana sipatani na majani”

Hata hivyo Harmorapa amefunguka kuhusu ishu hii na kukana kuwa wimbo huo unamlenga Majani. Harmorapa alikiri kuwa Sasa hivi Majani sio meneja wake lakini hii sio sababu ya kumdiss kwenye wimbo Kama wengi wanavyodai.

“Ni kweli kwa sasa P Funk Majani siyo meneja wangu, ila siyo kweli kwamba nimemdiss kwenye ngoma yangu, kwa sababu hatuko pamoja kikazi ila bado tuna mahusiano mazuri na hatuna ugomvi, wala hajawahi kunitimua hizo ni fununu tu. Ngoma yangu ya Ajitokeze ni ngoma inayonizungumzia mimi, kwamba hakuna anayeweza kutokea akawa kama mimi na kama yupo basi ajitokeze, ila siyo dongo kwa Majani,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua