Harmorapa- Nimeumizwa Sana na Kitendo Cha Wema Kutangaza Ndoa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Harmorapa amefunguka na kuweka wazi kuwa hisia zake zimeumizwa baada ya mwanamke anayempenda kutangaza Kuolewa na mwanaume mwingine.

Harmorapa ambaye amekuwa muwazi tangia Mwanzoni kuwa anampenda Wema na kutamani kuwa naye kimapenzi ameonekana kukata tamaa ya kuwa naye baada ya Wema kutangaza ndoa na mpenzi wake PCK.

download latest music    

Harmorapa ameeleza kuwa labda haikupangwa kwa yeye kuwa na Wema Sepetu ndio maana hadi sasa hajafanikiwa kuwa naye, hivyo amenyoosha mikono juu kuhusu hilo.

Siku chache zilizopita Wema alimuanika hadharani mpenzi wake PCK na kumuita Mume wake mtarajiwa lakini pia PCK amekiri kuwa anategemea kumuoa Wema hivi na inasemekana kuwa hivi sasa Wema yupo nchini Burundi kwa ajili ya kutambulishwa kwa ndugu wa PCK.

Kama Utakumbuka kuwa kwenye uzinduzi wa movie mpya ya Wema Sepetu, D.A.D uliofanyika Mlimani City wiki kadhaa zilizopita Harmorapa aliibuka na kumkabisha Wema zawadi ya ua kama ishara ya upendo wake kwake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.