Loading...

Hatimaye Lady Jay Dee Aonekana Kwenye Msiba Wa Ruge

March 05, 2019 at 06:07
Hatimaye Lady Jay Dee Aonekana Kwenye Msiba Wa Ruge

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee ameonekana kwa Mara ya kwanza kwenye msiba wa Ruge Mutahaba.

Kwa miaka mingi imekuwa jambo la wazi kuw Lady Jay Dee na Ruge hawaivi katika changu kimoja Lakini wengi walitegemea jambo hilo lingebadilika mara Baada ya Ruge kufariki.

download latest music    

Siku nne za mwanzo za msiba wa Ruge Lady JD hakuonekana kabisa katika msiba wala hakutoa pole Kupitia Mitandao ya kijamii jambo lililosababisha mashabiki kumjia juu.

Lakini Lady Jay Dee ameonesha kuwa amesahahu yote kwani siku ya jana ameonekana akiwa mkoani Bukoba akishiriki kumzika Ruge Mutahaba ambaye anazikwa mkoani Kagera.

Lady Jay ameonekana kwenye picha ya pamoja na msanii mwenzake wa Bongo fleva Mwana FA.

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…