Loading...

Hawa kutoka ‘Nitarejea’ alioshirikishwa na Diamond adaiwa kupotelea kwenye vileo!

July 17, 2017 at 17:24
Hawa kutoka 'Nitarejea' alioshirikishwa na Diamond adaiwa kupotelea kwenye vileo!

Nitarejea ni wimbo ambao bado unafanya vizuri Hata baada ya kuachiwa mwaka Wa 2013. Diamond Platnumz alimshirikisha muimbaji anayejulikana kama Hawa na kutokana na sauti yake nzuri, mrembo huyu alitarajiwa kwenda mbali lakini hivyo sivyo mambo yalienda.

Hawa anasemekana kuwa alipata mtoto wake Wa kwanza anayedaiwa kuwa mtoto wa Diamond Platnumz na baadaye akafunga ndoa na mwanaume mwingine ambaye amemsababisha kuingilia vileo kutokana na ‘stress.’

Sasa hivi mrembo huyo amekiri kuwa maisha yake ilipotelea kwenye unywaji wa pombe kali aina ya gongo, kiasi cha kumfanya apoteze mwelekeo maishani mwake.

Akizungumza na Global TV Hawa alisema kuwa alijipata kwenye maisha haya baada ya mumewe kuondoka na kumuacha bila mawasiliano yoyote kwa muda wa miaka miwili baada ya kukaa kwenye ndoa yao kwa muda mfupi.

Kutoka na kufikiria sana, Hawa alitafuta namna ya kutoa ‘stress’ na akaingia kwenye vileo ambavyo vimemdhoofisha kimwili. Amedai kuwa amekonda huku akiomba msaada kutoka kwa mashabiki na wadau kumsaidia kuepuka maisha haya ambayo yanampeleka vibaya.

 

Leave a Reply

Be the First to Comment!

avatar
wpDiscuz

in Entertainment
Loading...
I write entertainment stories as well review and critic local music. Apart from my busy schedule you can catch me on social pages by clicking on them below