Hemed Phd Akiri Kuwa Msanii Mwenye Watoto Wengi

Kuna tabia za wasanii hazibadiliki tena hasa Kwa wasanii wa kiume, wengi wamekuwa  wakikataa kuwa na majukumu  hasa ya kifamilia(watoto), kuwa na watoto sio jambo dogo , lakini pia sio jambo la mkosi, kuwa na mtoto ni jambo la kheri, kuna baadhi ya wasanii wakubwa tu nchini wamekuwa  wakikata majukumu ya kulea watoto hao na kuwaachia  wazazi wa upande wa pili kubaki wakiangaika na mizigo ya kulea peke yao.

Hemed Phd ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha ‘Mkimbie’ anasema kuwa amekuwa kimya kwa muda kwa sababu ya majukumu ya kifamilia”tunakuwa kimya kutokana na majukumu,majukumu ndio yanaweza kukubadilisha kutoka kwenye ujana kwenda kwenye ubaba, siwezi kusema kuwa ni mafanikio sana kwa sababu havikuja katika mipango kama nilivyotarajia,, hivi vitu vilihappen tu buubaa basi  Mungu akafanya yake lakini ninajivunia kwa sababu ninaweza kuwahudumia  watu ambao wananiangalia kwa kiasi kikubwa .Am proud to be a father'” alisema Hemed

download latest music    

Msanii Hemed  Phd , alikiri kuwa hata yeye alikuwa akichomoa pale alipokuwa akiambiwa kuhusu taarifa za wanawake wake kumwambia wanaujauzito lakini inapokuja kwenye swala la mtoto anatoka amefanana nae kila kitu hivyo ni lazima akubali”kiukweli mwanzo nilikuwa nazingua  kwa maana ya kwamba nilikuwa sizikubali mimba kabisa lakini copy zilivyotoka,wanangu wazuri sana,wanangu wamenizidi uzuri ivyo inabidid tu niwakubali maana wanafanana na mimi’ anaendelea kuongea

Hemed anasema kuwa hata hivyo , imekuwa tofauti kwa upande wake kwa sababu watoto wake wote hakuna ambae amebambikiziwa hata mmoja wote ni wa kwake na anawalea wote,kwa sababu hata matendo ya kupata mimba  anavyofanya anakuwa anajua kipi kinafanyika.

Hata hivyo kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa pamoja na kuwa na watoto wengi lakini amekuwa akimpost mmoja tu” ni kweli ,lakini katika familia kuna mambo mengi, na bado ninayaweka sawa, yakikaa sawa ntawaweka wote , ila kwa sasa naomba ijulikana kuwa huyo ndo mwanangu na ifahamike ivyo kwa sasa” aliongezea Hemed

Kuhusu kuwa na watoto wengi hemed alipoulizwa ana watoto wangapi alijibu”ngoja nikatafute daftari langu kwanza niangalie idadi, ila nashukuru mungu tumeambiwa tuijaze Dunia kwaiyo kuwa na  watoto wengi ni sawa tu’ aliongezea Hemed

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.