Hii Ndio Sababu Kubwa Iliyomfanya Happiness Kuficha Sura Ya Mwanaye

Miss Tanzania mwaka 2001 Happiness Magesse au maarufu kama Millen amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa iliyomfanya mpaka akachelewa kuweka wazi sura ya mtoto wake King Kairo.

Millen alijifungua mtoto wake mwaka jana mwezi July lakini amemuonyesha mtoto wake mwaka huu mwezi wa machi ambapo alimficha sura yake kwa muda wa miezi tisa.

download latest music    

Wiki iliyopita Millen alianika sura ya mwanaye King Kairo kwa mara ya kwanza mtandaoni alipokuwa ametokea kwenye jarida la ‘Genievieve’ la nchini Nigeria.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo, Millen ameweka wazi kuwa sababu pekee iliyomfanya akamficha mtoto wake ni kutaka amuonyeshe katika muda sahihi na katika kipindi hiki au mwezi huu wa maadhimisho ya ugonjwa wa Endometriosis ambao umekuwa ukimsumbua kwa miaka mingi.

Nilikuwa na mpango ambao ulikuwa una muda sahihi, mtoto wangu ni sehemu kubwa ya stori yangu ya maisha yangu hivyo nilihitaji kumuonyesha during Endometriosis month mwezi huu machi”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.