Hii ndo sababu Elizabeth Michael ‘Lulu’ lazima ang’are kushika kila mtu kwenye sherehe yoyote

Muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameweka wazi kuwa yeye lazima apendeze zaidi kuliko mtu yoyote anapoenda kwenye sherehe yoyote ama ata akiwa katika kazi zake za filamu.

Sababu ya Lulu kupenda kupiga pamba ni kuwa anapenda kuvaa na kuonekana tofauti kila mara kwani kung’ara ndo jambo ambalo linampa furaha yeye.

download latest music    

“Mi napenda kupendeza kila wiki, kama nitatoka na kuwa sehemu iliyopendeza na nguo za kipekee kuna wakati nawatania rafiki zangu nikiwaambia waandae tu shughuli nije niwafunike kwa pamba kali,” alisema Lulu.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere