“Hii sio Tanzania Niliyoizoea, Tupaze Sauti”- Rose Ndauka

Muigizqji wa Bongo movie Rose Ndauka ni moja kati ya wasanii walioguswa na tukio la kinyama alilofanyiwa mwanafunzi Aqwilina Aqwline siku chache zilizopita na polisi.

Aqwilina ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo cha Usafirishaji (NIT) alifariki dunia baada ya kupigwa risasi na polisi kituo cha mabasi cha Mkwajuni Kinondoni ambapo polisi hao walikuwa wanawatawanya wafuasi wa Chadema Kitiona hapo na Aqwilina alikuwa anapanda basi kwa ajili ya kwenda kupeleka barua yake ya masomo Bagamoyo.

download latest music    

Rose Ndauka amefungukia suala hilo la kusikitisha na kueleza machungu yake kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika:

Enough is enough umefika muda sasa wa kuadress hili tatizo kama lilivyo without sugar coating it kwa namna yoyote! Recently kumekuwa na utumiaji mkubwa wa nguvu kusimamisha/ kuzuia / uhuru wa mawazo.Haya yamesababisha vifo ukosefu wa amani na furaha kwa Watanzania walio wengi kitu ambacho sio sawa, Amani ya Tanzania yangu na Watanzania wenzangu imekuwa mashakani na kama Amani inaanzia moyoni basi wengi wamekuwa waoga kusema hawana hiyo peace of mind. Huyu mwanafunzi ambaye hakuwa na uhusiano wowote wa tukio la jana kakumbwa na was umauti kwa kosa la polisi. Just one bullet stole a dream worth millions. Mungu akulaze pema mdogo wangu but this should be the beginning of the end of this brutality tupaze sauti kukemea suala hilo this is not the Tanzania am used to”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.