Holly Star Atamani Kuwa Zaidi ya Michael Jackson

Msanii Holystar amefunguka na kusema kuwa amekuwa na ndoto kubwa ya kutaka kufanya muziki ambao utatamba zaidi ya hapa Tanzania na kuwateka hata mashabiki nje ya Tanzania na Duniani kwa ujumla.

Holy star anasema kuwa ndoto zake ni kufanya muziki wake , kazi zake na jina lake kujulikana Dunia nzima na kuwa zaidi ya vile alivyokuwa akijulikana Michael jackson hapo awali.

download latest music    

Holy star anasema kuwa muziki wake sio kwa ajili ya watanzania tu na hata anapofanya kazi ya muziki amekuwa na malengo mengi ikiwepo na Kupata pesa, kujulikana sana,kuwa na maisha mazuri .Pia anasema analengo kuwa la  kuwa na jina ambalo akisimama jukwaani watu wanashangilia zaidi ya vile walivyokuwa wakifanya kwa Michael Jackson.

Holy star ambae kwa sasa ameachana na aliyekuwa mke wake Sister Fey , amefunguka pia sababu ya kuachana na mke wae huyo na kusema uwa alikuwa akiteseka sana pamoja na kwamba alikuwa akimtunza kwa kila kitu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.