Loading...

Huddah Agoma Kuwekwa Kundi Moja na Vera Sidika

September 14, 2018 at 14:45
Huddah Agoma Kuwekwa Kundi Moja na Vera Sidika

Socialite maarufu kutoka nchini Kenya Mrembo Alhuddah Njoroge maarufu kama Huddah Monroe amegoma kabisa kushindanishwa na hasimu wake Mrembo Vera Sidika ‘Queen Vee’.

Huddah amekataa kushiriki Tuzo za Black Entertainment Film Fashion Television and Arts (BEFFTA) ambapo yupo kipengele cha International Film and Fashion ambacho hasimu wake Vera Sidika pia amechaguliwa kushiriki na kusema kuwa hawezi kulinganishwa naye hata kidogo.

Loading...

Huddah na Vera wamekuwa Kwenye mvutano wa muda mrefu na hata kugombana kwenye mitandao ya kijamii na sasa Huddah amegoma kabisa kishiriki tuzo hizo kutokana kuwekwa kundi moja na adui yake.

Kupitia mitandao ya kijamii Huddah ameandika haya kuhusiana tuzo hizo:

Mmenichagua katika tuzo ambazo wala sizifuatilii kabisa nipo bize na mambo yangu na ninafanya mambo yanayonihusu na sipo kwa ajili ya kulinganishwa na hao mlioniweka nao, kwa Afrika sina wakulinganishwa naye yaani sijaona labda USA (Marekani), nipo bize na brand yangu ya HUDDAH na kuangalia vipi naikuza sitaki ushindani na mtu”.

Huddah na Vera wamekataa mara kwa mara kuwa na bifu lakini matendo yao yamekuwa yakionyesha utofauti.

5
Leave a Reply

avatar
5 Comment threads
0 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
4 Comment authors
lilianKarenLuvundoCharloCaramel Recent comment authors
newest oldest most voted
Caramel
Guest
Caramel

Upuzi

Charlo
Guest
Charlo

Maringo yote hayo na huna lolote

Luvundo
Guest
Luvundo

Nyote wadangaji kikubwa ni kipi

Karen
Guest
Karen

Hayatuhusu

lilian
Guest
lilian

Makubwa


in Entertainment

Loading…

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.