Huddah Monroe Awatolea Povu Zito Wasanii Wa Kenya

Socialite na mfanyabiashara maarufu nchini Kenya Huddah Monroe amefungukia Sakata la kampeni ya ‘Play Kenya Muzic’ Na kuwatolea Povu wasanii wa Kenya na muziki wao.

Nchini Kenya kwenye vituo mbali mbali vya Radio kumekuwa na kampenzi ya Play Kenya Music ambayo inashinikiza ma Dj na Watangazaji kupiga muziki wa wasanii wa kenya badala ya wasanii wa nchi nyingine zaidi.

download latest music    

Huddah Monroe amefunguka na kuweka wazi kuwa  anapenda sana kusikiliza nyimbo za wasanii wa Nigeria kuliko Kenya.

Huddah kupitia Instagram Stories, amesema kuwa muziki wa Nigeria unahusisha maisha halisi ya kwenye jamii. Huku akiuponda muziki wa Kenya ambao amedai kuwa nyimbo nyingi ni za mapenzi, zina sifia ulevi na madawa ya kulevya .

Unajua kwanini huwa huwa nasikilisa sana muziki wa Nigeria? unaniingia sana moyoni, kwa sababu nasikiliza kile kitu nataka kusikiliza, wenzetu wameamka sana. Ujumbe uliopo kwenye nyimbo zao sio tu mapenzi na madawa ya kulevya, bali wanazungumzia maisha halisia. Kiukweli wananivutia, na hivyo ndio vitu tunataka kusikia. Na sio kila siku kuimbia ngono, mapenzi na madawa ya kulevya”.

Lakini pia katika upande mwingine Huddah amewapongeza wasanii kama Nyashinski, Sauti Sol, Octopizzo na Khaligraph Jones kwa kufanya muziki mzuri na kuitangaza Kenya kimataifa .

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.