Hukumu ya Masogange Kutolewa February,21

Ni kama mwaka sasa unakaribia kuisha kwa baadhi ya wasanii wa muziki, movies na watu maarufu kuwa wakisota mahakamani kila siku kufatilia kesi zao zinazowakabili zidi ya madawa ya kulevya, moja kati ya watu hao ni Agnes Masogange ambae nae pia alikumbwa na sakata la kutumia madawa ya kulevya.

Hata hivyo mahakama ya Kisutu inayoshughulikia kesi yake imetangaza kuwa wameshakamilisha kila kitu kuhusu kusikilizwa kwa kesi hiyo hivyo hukumu yake itatolewa mwaka huu February 21 na hakimu  Wilbard Mashauri  baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na  costantine kakula  kuwaita mashaidi watatu na kutoa ushaidi wao  dhidi ya Agnes na kufunga jalada la kesi ili aweze kujitetea mwenyewe.

download latest music    

Hata hivyo katika kujitetea kwake ,agnes ambae alituhumiwa kwa matumizi ya madawa ya kulevya aina ya heroine anasema kuwa hajawahi kutumia madawa ya aina yoyote hata siku moja  nakusema kuwa ukiachana na kazi yake ya usanii yeye ni mfanyabiashara wa nguo.

Agnes akielezea mazingira ya kukamatwa kwake siku ya tuko ni kwamba yeye mwenyewe hakuwepo nyumbani alikuwa ametoka iula alimwacha dada yake numbani ambapo mapolisi walipokuja waliamua kumuweka dada yake chin ya ulinzi na kumlazimisha kumpigia yeye simu na kusingizia kuwa anaumwa ili aweze kurudi nyumbani.

Agnes alisema kuwa hata aliporudi nyumbani alikutana na maaskari na walikuwa walishafanya upekuz lakini hawakukuta kitu chochote lakini walipomaliza upekuzi walimkata na kumchukua kumpeleka kituo cha polisi.

Kesi ya Agnes inatarajiwa kutolewa hukumu mwezi huu hivyo itakuwa imebaki kesi ya madawa ya kulevya inayomkabiri Wema Sepetu na wenzake.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.