Husna na Tunda Ndani Ya Sakata La Kuibiana Mwanaume

Mlimbwende aliyewahi kushiriki shindano la Miss Tanzania miaka ya nyuma Husna Maulid na video vixen maarufu Bongo Tinda Sebastian wamedaiwa kutibuana kisa bwana wanayemgombania.

Gazeti la ijumaa wikienda linaripoti kuwa Husna ambaye alikuwa na urafiki na Tunda alijikuta amesalitiwa na shoga yake huyo baaada ya kugundua kuwa amemchukulia bwana ake anayeitwa Ally.

download latest music    

Katika mahojiano aliyofanya na Gazeti hili, Tunda alisema watu wamekuwa wakizungumza sana kuhusiana na hilo kwamba ameibiwa bwana na rafiki yake Tunda kitu ambacho hakifahamu kwani anachojua yeye ni kwamba ana mpenzi wake mmoja tu anayejulikana kwa jina la G na ndiye rafiki yake pia.

Jamani naomba watu waelewe kwamba nina mpenzi wangu anaitwa G, huyo mwingine anayetajwa simjui na wala sina urafiki na mtu zaidi ya mpenzi wangu, huyo ndiye rafiki yangu wa karibu“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.