Husna Sajent Na Wolper Mambo Safi.

Wanadada wawili waliokuwa mahasimu wakubwa kutokana na kutembea na bwana mmoja kwa sasa wameamua kuweka mambo yao sawa na kuwa marafiki kama zamani kwa sababu yule aliyekuwa akiwafanya wagombane hayupo tena.

Kitendo hichi kimejidhihirisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mwanadada Jackline Wolper ambapo alimuhalika mwanadada huyo na alihudhuria .Husna Sajenti na Jackline Wolper walikuwa kuwa maadui wakubwa baada ya Husna Sajent kutoka kiapenzi na aliyekuwa mpenzi wake na Jackline ambapo wawili hao waligombana kwa ajili ya mwanaume huyo.

download latest music    

Msanii  jackline wolper

mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la  Mwami Radjabu  inaesemekana ni mkongo alifikia hatua ya kumvalisha pete husna sajent lakini hawakubahatika kufunga ndoa na mwanadada huyo.

Hata hivyo moja ya watu wa karibu wa Husna Sajenti alisema kuwa wawili hao waliamua kuacha kugombana kwa sabau husna tayari alishaachana na mwanaume huyo na wameona kuwa hakuna haja ya wao kugombana ukizingatia wao wote ni wanawake.

Tulishamaliza tofauti zetu,sian tofauti  wala bifu na  Jackline, maana aliyekuwa anatugombanisha ni mwanaume na hayupo tena na sisi ni wanawake  na tujifunze kuwa wanaume ni watu wa kupita. Aliongea Husna Sajent

Hii itakuwa funzo pia kwa wasanii wngine hasa wa kike ambao wamekuwa wakiingia katika mabifu hovyo hovyo kwa sababu ya wanaume bila kujali maslahi ya urafiki wao kwanza.wasani wengi wa kike wamekuwa wakiingia katika migogoro kwa sababu ya kuibiana wanaume.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.