Idris aeleza kwanini Wema Sepetu hakuenda kwenye uzinduzi wa viata vyake ‘SultanXforemen’

Idris alihudhuria uzinduzi wa filamu ya Wema Sepetu ‘ Heaven Sent’ ambayo ilifanyika Mlimani City takriban wiki moja hivi.

La kushangaza ni kuwa Wema Sepetu hakuhudhuria uzinduzi wa viatu vya Idria zinazoitwa ‘SultanXforemen’. Uzinduzi wa viatu hivyo uliudhuliwa na mastaa kadhaa akiwemo Iren Uwoya, Gabo,Selin, Mc Piilipili, Ally Rehmtullah,Quick Raka lakini Wema Sepetu hakuonekana.

download latest music    

Idris alidhibitisha kuwa alimualika Wema Sepetu kwa uzinduzi huo. Mchekeshaji huyo alifunguka na kusema kuwa alimpigia simu Wema ambaye alimpa sababu ya yeye kushindwa kuja kwa uzinduzi huo.

“Nilimualika Wema sema unajua nyie wanawake mambo yenu hivyo ameshindwa kuja ikabidi ni mpe ridhaa, wakati naongea naye kwenye simu alivyosema sitaweza kufika basi nikamjibu uliza kiatu,” amesema Idris.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere