Loading...

Idris afunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na tuhuma za “kufilisika”

September 08, 2017 at 21:25
Idris afunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na tuhuma za "kufilisika"

Kumekuwa na tetesi nyingi kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Tsh. milioni 500 alizoshinda Idris kupitia Big brother mwaka 2014, Watu wengi wakiwemo wasanii kama Ney wa Mitego alimtuhumu kuwa “amefulia” huku wengi wakiamini alizitumia pesa hizo kwa starehe na wanawake.

Katika mahojiano alioyafanya jana Idris na “Dizzim online” aliweka wazi kuwa hakufilisika kwa kuhonga pesa zake kwa wanawake na kupenda starehe kama watu wengi walivyokuwa wanadai bali aliitumia kiasi kama cha shilingi milioni 50 kuwekeza kwenye biashara  ya madini ya almasi ambayo aliishia kutapeliwa na kupoteza pesa nyingi sana.  Pia aliweka wazi shida zote alizopitia hadi kuishiwa kiasi cha kushindwa kulipia bili ya umeme, maji na gharama nyingine na hadi kwenda kuomba hifadhi kwa marafiki ambapo marafiki ili aishi kwa muda wengine walikataa kumpa msaada ambao alikuwa anawasaidia kipindi ni milionea  na ana uwezo kifedha,

download latest music    

Idris alisisitiza kuwa kisa cha yeye kuishiwa kabisa ni kuwekeza nusu ya utajiri wake huo katika  kuandaa brand yake ya viatu Sultan by Foremen na ikabidi asubiri kwa jumla ya miaka miwili kwa bidhaa hiyo kuwa tayari. Idris alikanusha vikali tetesi zilizoenea kuwa mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu ndiye alikuwa chanzo cha yeye kufilisika na kudai kuwa hakutumia pesa yake kwa starehe bali tu ilikuwa ni uwekezaji mbaya kwa muda ule pia anategemea kurejesha utajiri wake kwa brand yake mpya ya Sultan by Foremen.

Loading…

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment