Idris ajibu madai kuwa amerudiana na Wema Sepetu baada ya kuonekana pamoja Milimani city

Wema Sepetu na Idris Sultan waliachana mapema mwaka jana miezi michache tu baada ya mrembo huyo kupoteza ujauzito wake. Wema alikua amepachikwa mimba na Idris.

Jumamosi hii Agosti 26 Wema na Idris walionekana wakiingia Milimani city wakiwa pamoja. Staa hao wawili walihuduria uzinduzi wa filamu ya ‘Heaven Sent’ iliyofanyika Milimani city mall.

download latest music    
Wema Sepetu na Idris walivyo wasili Milimani City

Tokeo ya Wema na Idris kuingia ukumbini wakiwa pamoja ulizua madai kuwa wapenzi hao wa zamani wameamua kurudiana ndo sababu ya ‘kutangaza’ mapenzi yao hadharani.

Ata hivyo Idris alikana madai hayo alipohojiwa. Mchekeshaji huyo aliweka bayana kuwa kwa sasa hayupo katika mahusiano na mtu yeyote.

“Mimi siko na mtu yeyote kimahusiano, am single. Niliona amepost kuwa anataka date mie nikasema nampitia kwa hiyo sikuwa na haja ya kuomba date wala nini nikasema maana mzuri nampitia, kwa bahati nzuri nikakuta hamna mtu aliyempitaia huwenda waliokuwa anatolewa baru,” Idris alikiri.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere