Idris Sultan Alamba Shavu Nono Kutoka Kwa Uber

Mchekeshaji maarufu nchini Idris Sultan amelamba shavu nono siku za hivi karibuni baada ya kuchaguliwa kuwa balozi wa Uber.

Idris ambaye alijizolea umaarufu mwaka 2014 baada ya kushinda shindano la Bog brother Africa amezidi kung’aa siku za hivi karibuni baada ya kuendelea kupata madili kibao.

download latest music    

Idris alitangazwa rasmi wiki iliyopita na kampuni hiyo ambapo Meneja masoko wa Uber kanda ya Africa mashariki, Bi. Elizabeth Njeri amesema kampuni hiyo ilifanya utafiti kwa miezi kadhaa ili kujua nani atawafaa na Idris ameonekana sahihi kwao kutokana na mtindo wake wa maisha.

Idris amekuwa akifanya vizuri sana katika siku za hivi karibuni kwani mbali ya kuwa balozi wa Uber amepata mafanikio kadhaa Ikiwa ni pamoja kuchaguliwa kucheza Movie zaidi ya mbili kubwa nchini Marekani, Hollywood.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.