Loading…

Idris Sultan Amefunguka Mazito Kuhusiana Na Kifo Cha Kanumba

November 14, 2017 at 08:53
Idris Sultan Amefunguka Mazito Kuhusiana Na Kifo Cha Kanumba

Mchekeshaji na muigizaji wa Bongo movie, Idris Sultan amefunguka na kuandika mazito kuhusiana na kifo cha muigizaji wa Bongo movie Steven Kanumba.

Siku Jana muigizaji na mpenzi wa zamani wa Kanumba, Elizabeth Michael alikutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Kanumba na kutupwa jela kwa miaka miwili. Baada ya hukumu hiyo watu mbalimbali hasa wasanii wa muziki na filamu walijitokeza kuongelea kuumizwa huko kwa Lulu kufungwa.

Loading...

Idris alifunguka sio tu kuumizwa kwake kwa kifungo cha Lulu bali na kifo cha Kanumba kilichotokea miaka mitano iliyopita. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Idris alimuandikia Kanumba Barua ya wazi:

Dear Kanumba, Najua ulikuwa hunijui ila nilitembea kwa miguu toka Mbezi Kimara mpaka Kinondoni kuja kukuzika. Ni muda mrefu sasa umekuwa ukitembea na sisi kuomba upumzishwe, sasa naamini utapumzishwa kabisa. Allah akufanyie wepesi na milele utabaki moyoni mwetu. Tulifunga njia, na hata kuhema vizuri wengine tulishindwa na wengine hata depression tukapata kubwa sana yote kwa sababu ulitugusa sana katika mfano usizoeleka Naamini sasa haki yako sasa imepatikana na ninamuombea sana mama yako apewe nguvu na amani ya moyo, finally rested. Ni Mimi wako katika matumaini ya urithi wa ufalme wa movie Tanzania, Idris Sultan”.

 

Comments

  1. Inauma kwa kweli

  2. Yan kesi hii imekua ngumu sana

  3. Mola amlaze mahala pema

  4. Ilikua siku ndefu sana

  5. Mola mpe Lulu nguvu ya kuyapita haya maana hatujui nini kilitokea

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...
wavatar

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.