Loading...

Ikiwa Ni Kumbukumbu Ya Kifo Cha Juma Sajuki,Fahamu Historia Yake kwa Ufupi .

January 03, 2018 at 14:27
Ikiwa  Ni Kumbukumbu Ya Kifo Cha Juma Sajuki,Fahamu Historia Yake kwa Ufupi .

Sajuki alizaliwa mwaka 1984, mkoani Songea na kupata elimu yake ya msing na sekondari hukohuko mkoani Songea.Ambapo mwaka 2005 aliweza kuhitimu elimu yake ya kidato cha nne .

Katika kutafuta maisha kama kijana aliamua kuja mkoani Dar Es Salam mwaka 2005 , ambapo katika kusaka saka alianza kujulikana baada ya kuighiza filamu ya revenge aliyoshirikishwa na Ray Kigosi.baada ya hiyo ilimfungulia njia na kuonekana katika filamu nyingine nyingi kama Two brothers na Deogrtius Shija na  na ile ya Victoria.

Loading...

Akiwa katika kuigiza filamu ya Two brothers, Sajuki alikuta na Wastara  ambapo ukiachana na kufanya kazi pamoja lakini wajiingiza kwenye mapenzi yaliyopelekea kheri ya kufikia hatua ya kufunga ndoa.

Sajuki na Wastara mke wake enzi za uhai wake.

Mwaka 2009 wiki moja kabla ya ndoa yake mkewe wastara alipata ajali ya pikipiki wakiwa nae na kusababishwa kukatwa kwa mguu wa Wastara, lakini hii haikubadilisha ndoa ya wao kuoana kwa sababu walifunga ndoa wakiwa katika kiti cha wagonjwa.

Mke wa marehemu Sajuki siku ya ndoa yao.

Mnamo mwaka 2011,Sajuki alianza kuugua na kutibiwa katika hospitali TMJ,  na baadaye alihamishiwa muhimbili ambapo aligundulika kuwa alikuwa na uvimbe tumboni.baada ya uchunguzi wa muda mrefu na matibabu ilibidi kupelekwa india kwa matibabu zaidi ambapo aligundulika kuwa alikuwa na saratani ya ngozi na upungufu wa damu.

Hali ya Marehemu Sajuki akiwa mgonjwa

Alipewa dawa za kutumia  kuambiwa kuwa atatakiwa kurudi tena baada ya miezi kadhaa lakini mauti yalimkuta akiwa katika maandalizi ya kurudi India.

Sajuki alifariki January 2 ,2013 na mpaka marehemu anafariki alikuwa ameacha mjane na mtoto mmoja wa miezi kumi.

 

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…