Loading...

Irene Uwoya Amkwapua Bodyguard Wa Diamond

October 12, 2018 at 11:02
Irene Uwoya Amkwapua Bodyguard Wa Diamond

Muigizaji wa filamu za Kibongo Irene Uwoya ameonekana akiwa na Bodyguard maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Mwarabu Fighter.

Mwarabu Fighter alijizolea umaarufu alipokuwa mlinzi binafsi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz lakini aliacha kazi kwake mapema mwaka huu baada ya kutibuana.

Loading...

Uwoya ambaye amekuwa akitengeneza sana headlines Kwenye mitandao ya kijamii siku mbili hizi amerusha video iliyomuonyesha akiwa na Mwarabu fighter kazini.

Uwoya kuonekana na Bodyguard kama Mwarabu Fighter kumezidi kuzusha tetesi za kuwepo Mkono wa Kigogo ambaye anasimamia maisha ya gharama anayoishi Uwoya kwa hivi sasa.

Baadhi ya wasanii ambao wameonekana na walinzi wao binafsi katika siku Hizi za karibuni ni pamoja na Jacqueline Wolper na msanii wa Bongo fleva Barnaba Boy.

Share

Comments

  1. Jiheshimu we mama

  2. Daaaah umezidi sasa

  3. Unaudhi yaani ungejua tu

  4. Kwa raha zake mwenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…