Irene Uwoya Amtuhumu Dogo Janja Kwa Kuchepuka Kwenye Ndoa Yao

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali anaye trend kwa kiasi kikubwa hivi sasa Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa mume wake staa wa Bongo fleva Dogo Janja amewahi kuchepuka.

Aiku za hivi karibuni Irene Uwoya na Dogo Janja wamekuwa Kwenye headlines za Media mbali mbali huku tetesi zinazopamba moto ni kwamba ndoa yao inapumulia mashine.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Uwoya amefunguka baada ya kuulizwa maswali kadhaa kuhusiana na ndoa yake:

 

Swali la kwanza – Ni kweli mmeachana na Dogo Janja ?….. Irene alikataa kulijibu na kusema uliza swali lingine,

Swali la pili – Ni kweli hamkai pamoja na Dogo Janja ?…….Irene alikataa pia kulijibu na kusema uliza lingine

Swali la tatu – Ni kweli Umemu-Uniffolow Dogo Janja Instagram …? Irene alijibu “Hapana”

Swali la tatu – Ni kweli mnategemea mtoto na Dogo Janja….. Irene alikataa kulijibu na kusema Swali lingine

Swali la nne – Ni kweli Dogo Janja alishawahi kuchepuka kwenye ndoa yenu ?….Irene alijibu “Ndio”

Swali la tano – Ni kweli Irene Uwoya alishawahi kuchepuka kwenye ndoa yake ?…… Irene alijibu “Hapana”

Lakini mahojiano hayo Uwoya alifungukia skendo ya kupelekwa Nchi za nje Kula bata na mwanamume mwingine na kisha kumuacha Mumewe nchini.

Yeye kuonekana yuko nje ya nchi akionekana anakula bata bila Dogo Janja,Kila mtu anazungumza kile anachohisi kuzungumza na mimi siwezagi kuongelea mambo yangu kwenye media, Mimi kuonekana nje niko kwenye biashara zangu mbona Dogo Janja akiendaga kufanya video za nyimbo zake mfano Afrika ya Kusini hanibebagi ? kwahiyo mimi naendaga kibiashara kama yeye anavyoendaga kikazi”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.