Loading...

Jacqueline Wolper ajibu wanaosema amenyakua mume wa mtu

July 14, 2017 at 15:41
Jacqueline Wolper ajibu wanaosema amenyakua mume wa mtu

Inasemekana kuwa mpenzi mpya wa Wolper anayejulikana kama Brown ni mume wa mtu. Wolper amekemewa kwa tendo lake la kupora mume wa mtu.

Hata hivyo muigizaji huyo wa filamu ya Bongo amewajibu wanaomsuta kwa kusema kuwa mtu yeyote anayedai kuwa Brown ni mume wa mtu ajitokeze hadharani kuliko kusema mitandaoni.

Soma pia: Picha 10 za mpenzi mpya wa Jacqueline Wolper

Akiongea na Amani, Wolper alisema madai mitandaoni ni ya upuzi kwani hakuna mtu aliyeibuka na kusema Brown ni mumewe kabla ya yeye kuanza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Brown.

Jacqueline Wolper na Brown

“Kinachonishangaza ni kitendo cha mimi kuwa naye tu ndiyo watu wanaanza kuibuka na kusema eti ana mke, duh! Mbona kipindi siko naye, hakuna mwanamke ambaye alikuwa anasema ni mumewe. Sasa basi kama kuna mwanamke ambaye anadai ni mumewe ajitokeza hadharani. Nilichogundua baadhi ya wanaoibuka ni wale ambao waliwahi kuwa naye kitambo, sasa nasema hivi, huyo anayesema ni mume wake basi ajitokeze,” alisema Wolper.

 

Leave a Reply

Be the First to Comment!

avatar
wpDiscuz

in Entertainment
Loading...
Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere