Jacqueline Wolper: Msituchukulie Poa Bongo Movie

Muigizaji wa Bongo movie maarufu kabisa jacquiline Wolper amewataka wabongo wote hasa wale watu wenye tabia ya kuiponda Bongo movie wasiwachukulie poa kwani wanarudisha heshima yao hivi karibuni.

Kwa muda mrefu Sanaa ya Bongo movie Imesemwa kuwa imekufa na kila mmoja kuinyoshea kidole kwa kukosa ubunifu ambao ni muhimu ili kusaidia kuipeleka mbele ili kuhakikisha inakuwa na kufika level za kimataifa zaidi.

download latest music    

Ni kawaida siku hizi kusikia watu wakiiponda Bongo movie hasa inapofika wakati kuwa kuna makosa kadhaa ya kiubunifu yanafanyika. Imefika kipindi imekuwa hata ni kama soko Lao limekufa kwani sio sawa na miaka mitano nyuma.

Jacquiline Wolper ni moja ya msanii wa kike aliyejipatia umaarufu wake kutokana na kuchepuka filamu kadhaa za Bongo movie ambazo zilimletea umaarufu lakini hivi karibuni imekuwa ni nadra sana kuona wasanii hawa wanacheza filamu zao kutokana na soko Lao kupotea.

Wolper amefunguka na kusema sio kweli Bongo movie imekufa bali ni ilikuwa imelega tu ila hivi sasa wamepata madirector wapya hivyo wanategemea kurudi Kwenye chati kama zamani, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika haya:

Oya msituchukulie poa Bongo movie hii ndio class yetu na tunapeta kazi zinafanya zituweke mjini msidharau jamani…kwanza nasikia Bongo movie tumepata director mpya tutarudi tu chatini”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.