Jacqueline Wolper: Nitukane mimi usitukane damu yangu

Jacqueline Wolper ametoa onyo kali kwa wanaopenda kumkemea. Staa huyo wa filamu za Bongo amesema kuwa yuko tayari kuenda jela kwasababu ya kupigania wazazi wake.

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, Wolper alisema kuwa yeye huwa mpole kwa kawaida lakini mtu akijaribu avuke mpaka na kuguza familia yake hapo ndo kichaa chake huamka.

download latest music    

Mrembo huyo alieleza kuwa huwa haweki familia yake kwa Instagram kwasababu hataki wahusishwe na mambo yake, alitoa onyo kwa kusema kwamba mtu yeyote atakaye tusi familia yake ataona cha mtema kuni kwani yeye haogopi jela.

“Kwa mimi binafsi Jackline Wolper ni mpole, lakini ukija kwenye issue za wazazi mi nitaenda Segerea, ndiyo maana hujawahi kusikia Jackline Wolper kamuweka mama yake au baba yake kwenye instagram, kwenye Tv, yani sitaki wazazi wangu wahusike, nitukane mimi usitukane damu yangu, au usitukane mtu aliyenileta duniani, yani dakika sifuri nitapelekwa tu jela,” alisema Wolper.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere