Jaguar Akerwa na Tabia Alioonyesha Harmonize.

Jumamosi iliyopita msanii kutoka Tanzania Harmonize  alikataa kupanda jukwaani Eldoret baada ya madai kuwa Promoter alishindwa kumlipa salio lake kama walivyokubaliana kwenye mkataba. Hata hivyo tukio hilo limemuudhi Mbunge wa Starehe Jaguar kutoka Kenya ambaye pia ni mwanamuziki. .
.
“Ni tukio la kuhuzunisha lakini mimi NAMSHTUMU sana Harmonize….wakenya wamemsupport sana, wamesupport wasanii wa nje sana. Wengine wanatumia pesa zao kupiga simu, kurequest nyimbo zao. Mimi mwenyewe siwezi nikakosa kupanda stage sababu ya balance ambayo promoter amebakisha na ni kitu nilikuwa nafanya. Kwanza nadeal na mafans wangu. Kama Mimi ningekuwa Harmonize Saturday ningeenda kwa stage niambie watu samahani nimechelewa lakini kwa sababu mumenifikisha mahali nimefika saa hii mimi nitaperform lakini promoter hajanilipa…vitu zingine nitadeal nazo baadaye sababu bila nyinyi nisingekuwa Harmonize pale niko. Unapata kuna fans wametoka mbali hadi Eldoret kwa sababu yake. Sometimes unafaa kuangalia mafans kwanza,” alisema Jaguar. .
.
Akiongea kwenye Mambo mseto na  Mzazi willy Jaguar ametangaza kuwa wiki ijayo anawasilisha mswada bungeni utakaohakikisha kuwa wasanii wa Kenya pia wanapewa nafasi na kulipwa pesa nyingi kama wanavyolipwa wasanii kutoka nchi za nje. Vilevile, ameongeza kuwa yeye na wabunge vijana watashikana na kuhakikisha kuwa broadcasters wanatii sheria iliyopitishwa kuhusu kucheza 60% Kenyan content.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.