Jeshi la Polisi Wasisitiza Bado Wanamtafuta Mpenzi wa Wema.

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamesema wanamsaka mwanaume aliyeonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa na msanii Wema Sepetu.
Akizungumza leo Jumanne Novemba 6, 2018, Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo, Liberatus Sabas amesema polisi wanaendelea kumsaka mwanaume huyo na wakimpata wanamfikisha mahakamani.
“Polisi tunaendelea kumtafuta huyu jamaa, hatujakata tamaa na ikiwa tutamkamata lazima tumfikishe mahakamani kwani ana kesi ya kujibu,’’ amesema.
Amesema kwamba watu wanadhani labda jeshi la polisi limeshaachana na mwanaume huyo lakini bado ni mtuhumiwa na hivyo akikamatwa anapelekwa mahakamani.
ikumbukwe kuwa mwanadada wema sepetu na PCK walikuwa katika mahaba mazito yaliyotikisa mitandao ya kijamii na hata kufiki ahatua ya kutangaza  kufunga ndoa hivi karibuni,lakini ghafla kulizuka kwa tafrani kubwa kati yao na kusambaa kwa picha chafu na hata mwanaume huyo kutuhumiwa kumdhulumu wema pesa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.