Loading...

Joh Makini Akana Kupotea kimuziki.

February 13, 2018 at 07:21
Joh Makini Akana Kupotea kimuziki.

Msanii wa muzii wa bongo fleva kutoka katika kundi la Weusi John Simon maarufu kama joh makini amekana maneno na tetesi zinazozuka juu yake kuwa amepotea kimuziki na huku ikitajwa sababu kubwa kuwa ni wasanii wachanga wanaoibukia na kumfanya yeye kushundwa kusikika kama ilivyokuwa mwanzoni.

Joh mMakini ambae hivi karibuni ametoa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la  mipaka anasema kuwa watu wamekuwa wakiongea maneno bila kuwa na ushahidi kwa sababu hawaangalii vitu vingapi amekuwa akifanya kukuza muziki wake kwaiyo sio kweli kuwa anepozwa na wasanii wachanga.

Loading...

Sio kweli kuwa nimepoa kimuziki kama vile watu wengi wamekuwa wakisema ,wakizungumza na kuzusha katika mitandao ya kijamii, mimi niko vizuri na kazi zangu  ziko zinafanya poa kabisa  na ninachoataka kuwaambia cha zaidi ni kwamba sitgemei kuchuja hata siku moja.-Alifunguka Joh Makini.

Hivi karibuni Joh Makini alipata skendo ya kutembea na msanii mwenzake mimi mare lakini taarifa hizo walizikanusha na kusema ukaribu wao ni kama kaka na dada kwa sababu wamekuwa pamoja.

 

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.