Johari Afiwa na Mama Yake,Wasanii Wajitokeza Kumpa Pole

Msanii wa kike bongo movies nchi Johari Chagula amefiwa na mama yake mzazi siku ya tarehe 17 mwezi huu na msiba unafanyika nyumbani kwao jijini Dar Es Salam.Mama wa Johari ambae inasemekana kuwa alikuwa akiumwa kwa muda mrefu kidogo na kuwekwa hospitali kwa matibabu alipata umauti huo usiku wa kuamkia  siku ya jumatano.

Wasanii wengi wa filamu na muziki wamejitokeza kumpa pole msanii huyo kufuatilia tukio ilo la majonzi na la kusikitisha liliompa msanii mwenzao ,pia kwa ajili ya kumsindikiza mama wa Johari katika makao yake ya milele.

download latest music    

Akiongea na waandishi wa habari Jokate alitoa maneno ya faraja kumpa pole msanii mwenzake na kusema kuwa kilichobaki kikubwa kwa sasa ni kumuombea mama ambae anafarijika anapoona wasanii wengine wameenda kumpa pole mwenzao.

sis wote njia yetu ni moja , kikubwa ni kwa dada yetu Johari pole sana pole pole sana,lakini tnaendelea kumtumaini mungu maana mungu akikuita hauwezi kukataa.tumekuja wasanii wengi kwa ajili ya kumpa pole na kumpumzisha mama ayke na nina uhakika huko alipo mama anafurahi kuona wasanii tupo pamoja nae.

nae drcheni pia aliyekuwepo katika msiba pia aliongea na kulelezea majonzi yake kwa msiba huo na kusema.

Mungu ampe subira tu awe na moyo wa subira kwa sabau kuondokewa na baba kuna tofauti yake na kuondokewa na mama pia kuna tofauti yake kila mtu anajua , kuondokewa na mama ni kitu kikubwa sana tunajua machungu yake, tuendelee kumuombea Johari.

Nae Dogo Janja na mwenzie Irene Uwoya walionyeshwa pia kusikitishwa na msiba huo na kusema kuwa hili limekuwa pigo kubwa kwa Johari , kwa muda huu anahitaji sana ukaribu na watu ili aweze kukaa sawa.Hata hivyo Dogo Janja anasisitiza kumshukuru mungu kwa kila jmabo kwa sabau katika dini kifo pia ni ibada hivyo swala lililopo ni kumuombea marehemu.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.