Johari Akiri Kupata Raha Enzi Za Uhai Wa Ndikumana

Akiwa kama rafiki wa karibu wa msanii mwenzie , Johari Chagula amefunguka na kukiri kuwa enzi za uhai wa marehemu Ndikumana walikuwa wakila bata sana.Johari ambae ni rafiki wa karibu wa Irene Uwoya alisema kuwa kipindi Irene Uwoya  alipokuwa bado hajagombana na mumewe marehemu Ndikumana walikuwa wakila bata sana hasa pale Ndikumana alipokuwa akitoka nchini kwao akija Tanzania.

Johari anasema kuwa hata alipokuwa akija nchini alikuwa akija na zawadi nyingi kwa ajili ya marafiki wa karibu wa mkewe , na kuna kipindi mpaka waliweza kusafiri mpaka Cyprus kwa ajili ya kula bata tu na kurudi Tanzania.

download latest music    

kwakweli kama unavyojua mimi na Irene damudamu,Ndikumana alikuwa akitupa raha hatari hatari.Kuna wakati tulienda  naye hadi  Cyprus tukala raha sana.Kweli ndiku alikuwa na roho ya peke yake sana,Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.Alifunguka Johari Chagula

Ndikumana alifariki wiki iliyopita kwa ugonjwa wa moyo uliomkuta ghafla alipokuwa akiendelea na shughuli zake.hata hivyo sio wasanii wote wa bongo waliofanikiwa kuhudhuria katika mazishi yake kwa sababu hayakufanyikia nchini tanzania lakini familia ya Irene Uwoya pamoja na kwamba wawili hao hawakuwa katika maelewano mazuri kutokana na Irene kuolewa ndoa ya pili ya kiislamu kabla hata ya kuachana na Ndikumana  walifanikiwa kuona kaburi la msanii huyo.

Siku chache zilizopita, moja ya wadogo wa Ndikumana anaejulikanakama Laddy Ndikumana aliwatukana wasanii wa bongo movies na kuwahita wanafiki kwa kile kilichodaiwa kuwa kipindi marehemu yupo hai walikuwa wakila nae bata lakini marehemu amefariki hakuna aliyejitokeza katika msiba.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.