Jokate Ageukia Kwenye Uhandishi, Amwaga Sifa Kwa Raisi

Ni moja kati wa wasichana wa kitanzania aliopiga hatua kubwa sana katika sekta ya uchumi hasa kutokana na kujituma kwao.Alianza kwa platform ya urembo lakini baadae aliona fursa aliyoipata kwenye urembo inaweza kumfanya akaanzisha vipaji vingine vilivyo ndani yake.Jokate alianza kuwa mjasiriamali kupitia tasnia hiyo hiyo.

Kadri mafanikio yalivyozidi Jokate aliona anaweza kufanya urembo, biashara na bado akasaidia jamii yake katika mahitaji mbalimbali ya jamii yake, hivyo akaanza kusaidia sekta ya elimu kwa kuwapa hasa wasichana waliopo mashuleni vifaa mbalimbali kama mabegi,vitabu na hata baiskeli ili kuinua kiwango cha elimu kwa mtoto wa kike.

download latest music    

Lakini kumbe kuna baadhi ya walioona mchango wake katika jamii, Jokate aliteuliwa kuwa kaimu katibu mhamasishaji wa Chama Cha Mapinduzi yaani CCM, hii ilimuongezea Jokate fursa ya kukutana na watu mbalimbali hata kutambua matatizo yanayoikumba jamii yake kwa ujumla.

Ukiachana na urembo, ujasiriamali na kuwa mhamasishaji bora kwa vijana, lakini pia Jokate amekuwa ni moaj ya watu waliowahi kuingia katika tasnia ya muziki na wakafanya vizuri.Mwanadada huyo sasa amegeukia katika swala la uhandishi wa vitabu na makala.

Akiitambulisha kazi yake ya uhandishi katika ukurasa wake wa instagram, Jokate amesema kuwa sasa ameweza kuwa mwandishi ambapo katika kazi hiyo mwanadada Jokate ameandika maoni yake na kutoa  sifa za kumsifia raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. raisi John Pombe Magufuli na utendaji wake wa kazi akiwa katika kiti cha uraisi kwa miaka miwili aliyotimiza sasa.

 

 

Katika makala hiyo Jokate ameonyesha kazi mbalimbali alizofanya mheshimiwa raisi, uzalendo na utendaji kazi wake, mabadiliko kipindi cha awamu yake na misimamo mikali aliyonayo raisi katika kutekeleza kazi zake.Katika kazi yake hiyo Jokate amemfananisha raisi na nabii Mussa  anaepatikana katika vitabu vya dini.

 

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh. John Magufuli.

Jokate anazidi kuonekana mmoja wa wasanii na warembo waliokuwa wakijituma bila kusubiri mafanikio kutoka kwa watu wengine, anaweza kuwa ni msichana wa kuigwa wa watu wengine.

Jokate akiwa katika moja ya mikutano yake ya kiharakati.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.