Jua Njia za Kuondoa Msongo wa Mawazo (Stress)

Mara nyingi mtu anapokuwa na msongo wa mawazo anakuwa tofauti na vile alivyo na hata ufanyaji wake wa kazi unakuwa tofauti, kama ni kazini anakuwa mwenye unyonge na hata waliopo karibu yake umuona kuwa ni tofauti na vile alivyo.

vipo vitu vingi vinaweza kuleta msongo wa mawazo, ikiwa pamoja na

download latest music    
  • kuachwa na mpenzi au matatizo katika mahusiano
  • ugumu wa masomo,
  • kubanwa sana na kazi au matatizo kazini ,
  • marafiki,
  • hata ugumu wa maisha.

Mara nyingi inaqweza isiwe kawaida kwako kugundua haraka kuwa uko katika hali kama hiyo ingawa pia wapo wanaotambua na kutafuta msaada wa haraka kwa watu wao wa karibu, lakini dalili za mtu mwenye msongo wa mawazo ni pamoja na ;-

  • kulala sana bila mpangilio na isivyo kawaida
  • kutokupata usingizi kabisa hasa wakati wa usiku
  • kupoteza kumbukumbu ya vitu vingi
  • mabadiliko katika tabia yako ya kula
  • kuwa na hasira, kukataa tamaa na mara nyingi hata kujikuta unalia bila sababu.
  • mara nyingi unakuwa na wasiwasi na hujiamini.

Nini cha kufanya ili kuondoa msongo wa mawazo.

  • Jua nini sababu ya msongo wa mawazo kwanza na kisha jitahidi kwa kiasi kikubwa kuepukana na tatizo ilo, mara unapojua tatizo lako linasabbaishwa na nini itakuwa rahisi sana kupata muafaka wa tatizo ilo na hii itakusaidia hata unapotafuta ushauri kwa watu inakuwa rahisi kujielezea.
  • jifunze kusema hapana.-jitahidi sanakatika maisha kufanya kila kitu kwa kuangalia uwezo wako wa mwili na kila kitu pia, kama unaona kuwa kuna vitu viko nje ya uwezo wako kifedha, kiakili ,kimwili na hata maarifa ni bora kuachana nacho au kutafuta suluhisho na sio kulazimisha mambo.
  • wakwepe watu wanaokusababishia tatizo-kaa mbali na wale wanaosababisa ujionekuwa uko tofauti nao au uwezi kitu, kama ni mahusiano yanakwenda kombo sio lazima kuwa namahusiano kwa wakati huo ni bora kujipa muda na kujitafakari kabla ya kujiingiza huko tena, kama ni marafiki wanakupa mawazo basi kaa nao mbali kwa muda huku ukitafuta njia ya kuishi nao.
  • badilisha mazingira ya chanzo.-jitahidi kuyakwepa yale mazingira ambayo yanakupa mawazo muda wote, kama una pesa safiri na uwendembali kupumzisha akili yako, au jipe likizo hata ukatembelea sehemu tulivu peke yako ili  akili iwezie kupumua.
  • usijaribu kulikabili lile usiloliweza.-kama kuna kitu uweiz basi achana nacho sio lazima ukifanye wewe, fanya yale yanayowezekana kwa muda huo na kwa kiwango chako.

KUMBUKA;-hata siku moja usilee tatizo ambalo linasababishwa na msongo wa mawazo, watu wengi wamekuwa wakichukulia swala hili kama jambo dogo lakini mwisho wake unaweza kuwa na madhara zaidi ya unavyofikiri, kama unaona kuwa uwezi kutata basi ni bora kutafuta wataalamu wa mambo hayo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.