Loading...

Juma Nature afunguka kuhusu swala la kuchukiana na Chege Chigunda kwasababu ya mwanamke

April 20, 2017 at 16:02
Juma Nature afunguka kuhusu swala la kuchukiana na Chege Chigunda kwasababu ya mwanamke

Juma Nature ameongelea swala lililowafanya wengi kuamini kuwa hali sahani moja na Chege Chigunda. Msanii huyo mkongwe amekana kuwa mwanamke ndiye chanzo cha beef yake na Chege.

Cha kushangaza ni eti Nature hana beef yoyote na Chege; akizungumza katika kipindi cha eNewz ya EATV, rapper huyo alifunguka na kusema hajawahi kugombana na Chege.

Chege Chigunda

Jibu lake Juma Nature ni bainisho baada ya kuenea tetesi za kipindi kirefu zilikuwa zinawaaminisha watu kuwa mke aliyemuoa msanii huyo ndiye alikuwa mpenzi wa Chege hapo awali mpaka kupelekea kuimba wimbo wenye maudhui ya kumuaga mpenzi huyo uliyopewa jina la ‘Good bye’.

“Mimi sijawahi kugombana na mwanangu, sasa mimi nigombane na damu itawezekana kweli ?, hatuwezi kugombana, tutagombana stejini tu kwa sababu ya usanii lakini hatugombani kama hivyo unavyochukulia wewe”. Alisema Juma Nature.

Juma Nature

 

Leave a Reply

Be the First to Comment!

avatar
wpDiscuz

in Music
Loading...
Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere